FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA KISUKARI
Posted on: November 27th, 2019Fahamu zaidi kuhusu ugonjwa wa Kisukari
Kisukari jina la kitaalamu hujulikana kama diabetes mellitus ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya sukari katika damu.
Ugonjwa wa kisukari ni mlolongo wa matatizo mwilini ya mda mrefu na mfupi kutokana na upungufu au kutoweza kutumika vizuri kwa kichocheo kinachoitwa insulin.
Insulin hutengenezwa na chembechembe zilizopo ndani ya kiungo cha kongosho. Miili yetu inahitaji insulin ili kuweza kutumia sukari tuliyonayo mwilini.
Sukari inatokana na chakula tunachokula kila siku na hutumika kwa kuupa nguvu mwilini.
Kwa kawaida sukari ikizidi, ile ziada inahifadhiwa katika ini kama mafuta. Mafuta hayo hubadilishwa kuwa sukari na kutumika wakati tukiwa na njaa kwa mda mrefu. Endapo kuna matatizo ya kutengeneza au kutumika kwa insulin, sukari mwilini huongezeka haraka na inamaanisha ugonjwa wa kisukari upo na dalili kuanza kuonekana kama zifuatazo.
- Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.
- Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani.
- Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
- Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.
- Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
- Wanawake kuwashwa ukeni.
- Kutoona vizuri.
- Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
- Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole
- Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
- Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.
- Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
- Majipu mwilini.
- Kukojoa mkojo ambao mara baada ya dakika chache hujaliwa na sisimizi.
Mara uonapo dalili hizi wahi mapema hospitali kupima ugonjwa wa Kisukari kwa ni miongoni mwa magonjwa yanayochukua muda mrefu kutibika endapo mgonjwa atachelewa kupata matibabu, pia ni miongoni mwa magonjwa ambayo huua kwa kasi zaidi nchini.
Kuna nmana tofauti ya kujizuia kupata ugonjwa wa kisukari, ikiwemo kufanya mazoezi, kula vyakula vyenye afya kama matunda, mboga za majani na kula vyakula vyenye virutubisho vyote, na mwisho kujitahidi kupima kiwango chako cha sukari mwilini ili kujua kama kuna uwezekano wa kupata ugonjwa huo ili hatua zaidi zichukuliwe.
VIEPUKE VYAKULA HIVI VINASABABISHA KISUKARI...
UTAFITI mbalimbali uliokwishafanywa unaonyesha kuwa ugonjwa wa KISUKARI (DIABETES MELLITUS) unatokana na vyakula tunavyokula kila siku katika maisha yetu. Katika siku za hivi karibuni, ongezeko la ugonjwa huu limekuwa kubwa kwa sababau vyakula vinavyosababisha ugonjwa huu, ndivyo vinavyoliwa sana kuliko vile vinavyozuia.
Vyakula vingi vinavyotayarishwa kwa kukaangwa kwenye mafuta yenye moto mkali huwa na madhara kiafya na miongoni ma madhara hayo ni pamoja na kusababisha kansa ya kwenye mfuko wa uzazi. Vyakula hivyo ni pamoja na chips na vyakula vingine vinavyopikwa kwa kukaangwa kwenye mafuta.VYAKULA VYENYE CHUMVI NYINGI
Vyakula vyenye chumvi nyingi vimebainika navyo kusababisha kansa. Vile vile inaelezwa kuwa chumvi huwa kama chakula kwa bakteria wa kansa tumboni. Kansa ya tumbo inadaiwa kuua watu wengi nchini Japan kutokana na jamii hiyo kupenda sana vyakula vyenye chumvi nyingi. Miongoni mwa vyakula vyenye chumvi nyingi ni vile vya kusindika, kama vile nyama za makopo, maharage, n.kSUKARI
Matumizi mabaya ya sukari yanaelezwa kusababisha kansa. Kama tujuavyo, kuna aina mbalimbali za sukari lakini sukari hatari zaidi ni zile zinazowekwa kwenye vinywaji mbalimbali, zikiwemo soda, juisi za ladha ya matunda ambazo huwa na kiwango kingi cha ‘fructose’ ambayo inaelezwa kusababisha saratani ya kongosho.
Vile vile sukari kwa ujumla wake hairuhusiwi kutumiwa na mtu ambaye tayari amegundulika kuwa na kansa kwa sababu chakula cha chembechembe za saratani mara nyingi huwa ni sukari. Kwa matumizi mengine ya kawaida, sukari inatakiwa kutumiwa kwa kiwango kidogo sana katika vinywaji au vyakula tunavyotumia, tofauti na baadhai ya watu wanavyoweka sukari nyingi ili kupata utamu zaidi.NYAMA ILIYOIVA SANA
Upikaji wa nyama kwa muda mrefu na kwenye moto mkali (high temperatures) husababisha aina fulani ya kemikali inayojulikana kitaalamu kama ‘heterocyclic aromatic amines’. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Utah (University of Utah), umeonesha kwamba watu wanaopenda kula nyama zilizoiva sana, wako hatarini zaidi kupatwa na saratani ya njia ya haja kubwa (Rectal Cancer). Hivyo inashauriwa unapopika nyama, usipike kwenye moto mkali na kuiva kupita kiasi.
Unywaji wa pombe kupita kiasi nao unaelezwa kusababisha aina nyingi ya saratani, kwa wake kwa waume. Aina ya saratani zinazodaiwa kusababishwa na pombe ni pamoja na satarani ya mdomo, ini, utumbo na koromeo, ambazo ndizo zinazoua watu wengi hivi sasa nchini Marekani.NYAMA NA MAFUTA
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani, umegundua kwamba watu wanaopenda kula nyama kila siku wako hatarini kupatwa na saratani ya utumbo kuliko wale wanaokula mara moja moja. Pia baadhi ya mafuta ya wanyama na yale yanayowekwa kwenye ‘baga’ au ‘cheese’ huweza kusababisha kansa.
Vile vile ulaji wa vyakula vilivyotengenezwa kwa kuchanganya na nyama zilizosindikwa au kuhifadhiwa kwa matumizi ya muda mrefu husababisha saratani pia. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘soseji’ ambazo hupendwa na watu wengi. Pia mikate ya nyama ‘hot dogs’ nayo ni chanzo cha magonjwa ya saratani.
VYAKULA VYA UNGA MWEUPE
Vyakula vyote vinavyopikwa kutokana na unga uliokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake vyote na kuwa mweupe, vinaelezwa kuchangia magonjwa ya saratani kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘donati’ (doughnuts), maandazi, mkate mweupe, n.k
Mwisho, licha ya kuepuka ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu, unatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia vitokanavyo na mimea, mboga za majani na matunda kwa wingi kila siku. Utaona kwamba adui mkubwa wa afya zetu ni vyakula vyote vya kusindika na vile vya kutengenezwa viwandani au vile ambavyo wakati wa utayarisjaji wake huondolewa virutubisho vyake vya asili.