WATUMISHI HOSPITALI YA SEKOUTOURE WASHIRIKI MAFUNZO YA MEMIS.
Posted on: August 14th, 2022Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure wameshiriki mafunzo ya kidijitali ya mfumo wa MEMIS uliyofanyika kwa siku mbili na kuratibiwa na timu ya TEHAMA kutoka Wizara ya Afya.
Mafunzo hayo yamefanyika katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure kwa lengo la kuboresha na utumiaji sahihi kwa haraka wa miundombinu ya vifaa katika kutoa huduma kwa mgonjwa.
Lengo la mafunzo haya nia kuhakikisha kutoa huduma bora za utunzaji wa vifaa na wagonjwa.