SEKOUTOURE YASHIRIKI WIKI YA USALAMA BARABARANI

Posted on: March 14th, 2023

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure imeshiriki katika wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani inayoadhimishwa kitaifa Mkoani Mwanza katika uwanja wa Furahisha ambapo Mgeni Rasmi ni Mhe. Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Hospitali ya Sekoutoure imeweka Bnada la kutoa Huduma mbalimbali za Vipimo kama kupima uzito, Shinikizo la Damu, Elimu na Ushauri wa Rishe Bora, Vipimo vya Macho na Elimu ya Afya ya Akili.


Pia kitengo cha Damu Salama kanda ya ziwa kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa  Mwanza Sekoutoure wameendelea na zoezi la watu kuchangia damu kwa wadau mbalimbali na kusihi wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi katika uchangiaji damu kwani damu inasaidia kuokoa mahitaji ya wagonjwa mbalimbali wenye uhitaji.

Huku kauli mbiu ikiwa Tanzania bila ajali inawezekana timiza wajibu wako