SEKOU TOURE YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA UWT KWA KUTOA HUDUMA YA VIPIMO VYA KIAFYA

Posted on: January 27th, 2023

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza kupitia baadhi ya watumishi wa idara mbalimbali wameshiriki katika wiki ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi kwa kutoa huduma ya vipimo vya magonjwa mbalimbali.


Katika huduma ya vipimo vilivyotolewa ni pamoja na Kupima uzito, Kupima Shinikizo la Damu, Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wanawake, Homa ya Ini, Kupima Virusi vya Ukimwi, Uchangiaji damu, utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 na kutoa Elimu ya Bima ya Afya kwa Wote.