Prof. PASCHAL RUGGAJO AWASIHI WATUMISHI KUENDELEA KUFANYA KAZI KWA BIDII.
Posted on: October 20th, 2022Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya Prof. Paschal Ruggajo ametembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekoutoure na kukagua huduma za tiba na miundombinu mbalimbali hospitalini hapa na kufanya kikao na watumishi wa afya.
Katika kutembelea huduma za tiba amewaasa watumishi kutoa huduma bora na za kisasa zaidi kwa wagonjwa kwa sababu serikali inawekeza zaidi katika ununuzi, uendelezaji na usimikaji wa vifaa tiba na bora vya kisasa zaidi ili wagonjwa wapate huduma sitahiki.
Pia amewataka Madaktari kufanya utafiti juu ya magonjwa mbalimbali hasa magonjwa ambukizi yanayo hatarisha maisha katika jamii, hii itasaidia jinsi ya kujikinga matibabu na kuyaepuka kutokana na utafiti utakaofanyikana kusaidia kuielimisha jamii juu ugonjwa husika.