KATIBU TAWALA MSAIDIZI SEHEMU YA RASILIMALI WATU BW. DANIEL MACHUNDA AUNGA MKONO UTOAJI ZAWADI HOSPITALI YA SEKOU TOURE

Posted on: December 27th, 2022

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Rasilimali Bw. Daniel Machunda amejumuika na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure katika siku ya Sekou toure na kuwafariji mama mjamzito kwa kugawa zadi mbalimbali.

Pamoja na zawadi hizo Bw. Daniel Machunda amesema kuwa ni faraja kuwathamini wajawazito kwa kuwapa zawadi mbalimbali zitakazo wasaidia kabla na baada ya kujifungu kwani kujitolea ni jambo jema na lenye neema kubwa.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr. Thomas Rutachunzibwa ameushukuru uongozi wa hospitali kwa kumjali mama mjamzito kwa utoaji wa zawadi mbalimbali 

Kwa upande wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure Dr. Bahati Msaki amesema kuwa zoezi la utoaji zawadi na misaada mbalimbali kwa wagonjwa ni endelevu na kuendeleza huduma bora na za kisasa zaidi.

Zawadi hizo zimetolewa na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure.