KAMATI YA BUNGE INAYOSHUGHULIKA NA MASWALA YA UKIMWI, KIFUA KIKUU NA MADAWA YA KULEVYA IMEFANYA ZIARA KATIKA HOSPITALI YA SEKOU TOURE - MWANZA

Posted on: December 21st, 2022

Kamati ya bunge inayoshugulikia Ukimwi, Kifua kikuu na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana na Shirika la ICAP  wametembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure na kufanya ziara katika idara ya magonjwa ya akili na kuwajulia hali waraibu wa madawa ya kulevya.

Dr. Alice Kaijage amesema kuwa utumiaji wa madawa ya kulevya unaendelea kuathiri kwa kiasi kikubwa jamii ya sasa hususani vijana wanaojikita katika makundi mbalimbali na hii inachangiwa na kutojishugulisha na kazi mbalimbali hivyo basi kupitia kituo kitasaidia waraibu wa madawa kuacha matumizi ya madawa na kujikita katika maendeleo ya jamii.

Nae mbunge wa jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula amesema serikali itajenga nyumba kwa ajili yawaraibu wa madawa ya kulevya waishi ili kuondokana na makundi mbalimbali ya mitaani, pamoja na uangalizi mzuri wa wataalamu wa magonjwa ya akili kwani kituo hiki kinahudumia mikoa yote ya kanda ya ziwa.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali Dr. Bahati Msaki amesema kuwa kuwepo na idara ya magonjwa ya akili imesaidia sana kupunguza waathirika wa madawa kwani kwa kiasi kikubwa jamii inapata ufahamu juu ya madhara ya madawa ya kulevya na kuitaka jamii iendelee kutoa ushirikiano na Hospitali kwa ajili ya kuwaokoa vijana wengi katika wimbi la madawa ya kulevya.


Dr Meshark Samweli Mkuu wa idara ya Magonjwa ya akili amesisitiza jamii kutowafumbia macho waraibu wa madawa ya kulevya na kuwaleta hospitalini kupata huduma na kuanza kliniki dawa aina ya (Methadone).

Idara hii ya Magonjwa akili inahudumia na kutoa elimu juu ya madawa ya kulevya kwa mikoa yote ya kanda ya ziwa.